Nondo 5 za Kamala kwa Tanzania

HomeKitaifa

Nondo 5 za Kamala kwa Tanzania

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema nchi yake itaendelea kufanya kazi pamoja na Tanzania ili kuimarisha uchumi wa nchi na pamoja kuimarisha mahusiano ya kiuchumi baina ya nchi hizi mbili.

Katika kuhakikisha mahusiano hayo yanadumishwa na uchumi kukua, Kamala ametangaza mipango mipya mitano ambayo Marekani itatekeleza.

1. Benki ya mauzo ya nje itatia saini na kupata makubaliano na Tanzania ambayo yatawezesha hadi dola milioni 500 katika mauzo ya nje ya Marekani kwenda Tanzania. Katika eneo la usafirishaji, miundombinu, teknolojia ya dijiti na miradi ya nishati safi.

2. Ushirikiano mpya katika teknolojia ya 5G na usalama wa mtandao

3. Kujenga kituo cha kwanza cha aina yake katika bara hili, kituo cha usindikaji wa madini ambayo ni muhimu kwa kutengeneza betri za gari la umeme. Hii itashughulikia soko la kimataifa ifikapo 2026 kwani kazi inaendelea hivi sasa.

4. Zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 1 zinatarajiwa kupewa barani Afrika ili kuwawezesha wanawake, na Tanzania itanufaika.

5. Marekani kupitia USAID itatoa Dola za Kimarekani Milioni 1.3 kusaidia kukabiliana na Tanzania katika kukabiliana na mlipuko wa Marburg

error: Content is protected !!