Sabaya bado sana

HomeKitaifa

Sabaya bado sana

Hukumu ya Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake imeahirishwa hadi Juni 10, 2022,hii ni kutokana na Hakimu aliyepangwa kuisikiliza kuwa nje ya Mkoa kikazi.

Sabaya alikamatwa Mei 27, mwaka jana wilaya ya Kinonodni jijini Dar es Salaam na kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani Juni 4,2021 na kufunguliwa kesi mbili tofauti.

Katika kesi ya kwanza walihukumiwakifungo cha miaka 30 jela, hukumu ambayo Mei 6 2022 ilitenguliwa na Mahakama Kuu na kuwaachia huru baada ya kubaini dosari zilizojitokeza katika mwenendo wa kesi ya msingi katika mahakama ya chini.

error: Content is protected !!