Rais Samia alivyookoa fedha za sensa

HomeKitaifa

Rais Samia alivyookoa fedha za sensa

Kamisaa Mkuu wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda  amesema msimamo wa Rais Samia Suluhu umeokoa fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kugharamia kazi hiyo.

Makinda alisema mjini Kibaha kuwa wataalamu walimshangaza Rais Samia walipomweleza kuwa gharama za sensa ni takribani Sh trilioni tisa. 

Alisema baadhi ya watu waliomba zabuni ya kuifanya kazi hiyo kwa gharama kubwa, lakini Rais Samia alikataa.

“Mmoja aliomba kuhesabu watu kwa kutumia fedha za kiashi cha Dola za Kimarekani milioni tano, tukamuuliza uko sawa? Kwani unajua gharama ya sensa ni shilingi ngapi akasema hajui. Baadhi walifikiri hapo ni mahali pa kujipatia fedha kwamba ukimaliza utajenga majumba au utanunua magari,” alisema Makinda.

Makinda alisema baada ya wataalamu kumweleza Rais Samia gharama za kazi hiyo, alisema kwa kuwa sensa ya watu watafanya wananchi na asingetoa fedha hizo.

“Aliuliza tufunge shule na hospitali kwa ajili ya kufanya sensa akasema hapana haitawezekana kufanyika kwa gharama hizo, lakini itafanyika kwa gharama nafuu na watu watafanya wenyewe,” alisema Makinda.

Alisema fedha zilitumika zaidi kwenye mafunzo ya makarani na wataalamu wengine wakiwamo wa tehama na akabainisha kuwa watu wengi waliomba kuifanya kazi hiyo ili wapate fedha.

Makinda alisema baadhi ya nchi zimefurahishwa na kufanyika kwa sensa ambapo balozi wa nchi ya China alipongeza na nchi yake itasaini mkataba wa kutumia takwimu hizo katika masuala ya maendeleo.

 

error: Content is protected !!