Baada ya miaka 22 serikali yawalipa fidia

HomeKitaifa

Baada ya miaka 22 serikali yawalipa fidia

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA), imewakabidhi fedha ya fidia wananchi wapatao 50, waliokuwa wanaidai mamlaka hiyo kutokana na eneo ambalo serikali ilichukuwa miaka 22 iliyopita, kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji.

Wananchi hao walikabidhiwa fedha hizo Jumatano na kutakiwa kuondoka eneo la Mangamba Juu Manispaa ya Mtwara Mikindani, mkoani Mtwara ndani ya siku 90.

Mkurungenzi Mtendaji wa MTUWASA, Mhandisi Rejea Ng’ondya, ameshukuru serikali kwa kulipa fidia hiyo, huku akiwapongeza wananchi hao pamoja na serikali ya kijiji kuwa wavumilivu kwa miaka 22 kusubiria fidia.

error: Content is protected !!