Bara la Ulaya na uhaba wa mafuta

HomeKimataifa

Bara la Ulaya na uhaba wa mafuta

Wakati Bara la Ulaya likikumbwa na uhaba wa mafuta ya mawese, nchi ya Malaysia inajipanga kurejesha soko hilo baada ya wanunuzi kukwepa kununua bidhaa hiyo kutokana na masuala ya mazingira na kuingiza wafanyakazi kutoka nchi zingine.

Wauzaji wa maduka makubwa ya Uingereza, ambayo iliondoa mafuta ya mawese kutoka kwa chakula chake cha asili kuanzia 2018, wamelazimika kurejea kwenye bidhaa hiyo yenye utata katika miezi ya hivi karibuni kutokana na uhaba wa mafuta ya kula duniani uliosababishwa na vita vya Russia-Ukraine na Indonesia.

Waziri wa Viwanda na bidhaa wa Malaysia, Zuraida Kamaruddin amesema serikali yao itatumia nafasi hiyo kama fursa ya yakurejesha tena soko hilo la mafuta ya mawese kama hapo awali.

“Ni wakati wa sisi kuongeza juhudi za kukabiliana na propaganda mbaya za kudhoofisha uaminifu wa mafuta ya mawese na sisi kuonyesha faida nyingi za kiafya ambazo mafuta ya dhahabu hutoa,” alisema.

Zuraida alisema bei ya mafuta ya kula duniani huenda ikabaki juu katika nusu ya kwanza ya 2022 na mahitaji ya bara la Ulaya yanatarajiwa kuongezeka katika muda mfupi ujao kutokana na upungufu wa mafuta ya alizeti na soya.

Mafuta ya mawese yanatumika kutengeneza vitu kama lipstick hadi tambi, lakini wazalishaji wakuu wa Indonesia na Malaysia walikabiliwa na kususiwa baada ya kushutumiwa kwa kusafisha misitu ya mvua na kuingiza wafanyikazi wahamiaji kwa upanuzi wa haraka wa mashamba.

 

error: Content is protected !!