Rihanna kufungua duka Kenya

HomeBurudani

Rihanna kufungua duka Kenya

Mwanamuziki na mfanyabiashara, Robyn Rihanna Fenty maarufu kama ‘Rihanna’ ametangaza kufungua maduka ya vipodozi vyake vya Fenty Beauty katika nchi saba Afrika ikiwemo Kenya kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Ameeleza kufurahishwa na hatua aliyofikia na kuwa maduka hayo yatafunguliwa mwishoni mwa mwezi huu.

“nimeusubiria wasaha huu kwa muda sasa!! @fentybeauty & @fentyskin hatimaye wanafika AFRIKA!!! Botswana, Ghana, Kenya, Namibia, Nigeria, South Africa, Zambia, Zimbabwe…tunakuja Mei 27 na huo ni mwanzo tu!!!,” aliandika Rihanna.

Inakadiriwa kuwa hadi kufikia 2025 soko la vipodozi Afrika litakua kwa dola bilioni 1.26 kulingana na takwimu kutoka Datamonitor.

Kampuni hiyo ya vipodozi ya Fenty Beauty ambayo nusu yake inamilikiwa na Moët Hennessy Louis Vuitton (LVMH) yenye makao yake mjini Paris inajulikana kwa kuwa na vipodozi vyenye kufaa aina 50 za rangi ya ngozi (50 skin tones) , ikiwa ni pamoja na ‘dark shades’ zilizokuwa nadra ilipozinduliwa mwaka wa 2017.

Rihana mbaye kwa sasa anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mwanamuziki A$AP Rocky ndiye mwanamuziki wa kike mwenye pesa zaidi duniani na bilionea wa kwanza Barbados.

error: Content is protected !!