Fahamu mashirika 9 yaliyofutiwa usajili

HomeKitaifa

Fahamu mashirika 9 yaliyofutiwa usajili

Bodi ya uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini imefuta leseni za uendeshaji za mashirika tisa ya kimataifa na kitaifa ikiwemo taasisi ya Mo Foundation.

Taarifa ya Hajjat Mwantumu Mahiza, Mkurugenzi wa bodi hiyo iliyotolewa Oktoba 25, 20223 na kuchapishwa Novemba 13, 2023 inasema uamuzi huo umetokana na kikao cha bodi kilichofanyika mkoani Iringa.

“Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 7(1) (e) cha Sheria ya Mashirika yasiyo ya kiserikali Sura ya 56 ya Sheria za Tanzania…

…kupitia kikao chake cha 51 kilichofanyika tarehe 25 Oktoba 2023, mkoani Iringa inaujulisha umma kuwa mashirika yafuatayo yamefutiwa usajili wake kuanzia tarehe 25 Oktoba 2023,” inasomeka sehemu ya Mahiza.

Mashirika hayo ni pamoja na Mo foundation kutoka nchini Tanzania ambalo lilikuwa likifanya shughuli mbalimbali zenye tija kwa jamii ikiwemo ufadhili masomo ya ngazi za juu (Higher education), kusaidia watoto wenye saratani katika hospitali za vijijini pamoja na kusaidia upatikanaji wa maji safi vijijini.

Mengine Eyons & friends Tanzania na Fintrac, Arusha Poultry Keepers (APOKA) kutoka nchini Tanzania. Mashirika ya kimataifa yaliyofutiwa usajili ni pamoja Fintrac, UP4 Africa, Natural resource governance Tanzania, taasisi ya Agronomos sin fronteras, Raleigh Tanzania na Maliasili initiative.

Aidha, bodi hiyo imewekwa wazi kuwa orodha ya mashirika hayo ya kitaifa na kimataifa ni yale yalioomba kufutiwa usajili kwa hiyari.

Hata hivyo, bodi hiyo iliyopo chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Makundi Maalum haijaweka wazi sababu zaidi zilizofanya mashirika hayo kufunguwa shughuli zao nchini Tanzania.

NGO (Shirika lisilo la kiserikali) ni taasisi ya kijamii isiyofungamana na taasisi, dini au Serikali ambayo haina hisa katika mashirika mengine.

Lengo kuu la shirika hili, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ni kutatua changamoto zinazokwamisha maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

error: Content is protected !!