Kiwanda kipya cha vifunganishio kujengwa nchini

HomeKitaifa

Kiwanda kipya cha vifunganishio kujengwa nchini

Kiwanda cha Dongguan Chenghua Industrial Co. Ltd kinachotengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali zikiwemo za vyakula, mazao ya kilimo, urembo, vipodozi na vifaa katika sekta ya usafirishaji (logistics) kimepanga kufungua kiwanda kama hicho nchini Tanzania kutokana na kuvutiwa na fursa kilizoziona.

Mwenyekiti wa Kiwanda hicho Bw. Xiao Fei amesema uongozi wao umepanga kuja Tanzania kwa siku kumi kuanzia tarehe 19 Novemba na kukutana na Mamlaka ya Uwekezaji pamoja na kutembelea taasisi na masoko katika mikoa mbalimbali.

Hivi karibuni Serikali imebadilisha kanuni za uwekezaji ili kuwapa wawekezaji wapya na wale walio na nia ya kupanua biashara fursa sawa na pia imeboresha kanuni na kuzifanya kuwa rahisi kutekelezeka.

error: Content is protected !!