Ishara kuwa uliwahi kupata UVIKO-19

HomeElimu

Ishara kuwa uliwahi kupata UVIKO-19

Wimbi la ugonjwa wa UVIKO-19 limeathiri wengi duniani huku wengine wakionesha ishara za wazi za ugonjwa huo na wengine kutoonesha ishara zozote kabisa kutokana na kuwa na kinga mwili kubwa zaidi.

Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins ambao ndio wamekuwa wakiweka rekodi ya dunia ya idadi ya wagonjwa kwa kila nchi, vifo vilivyorekodiwa pamoja na idadi ya chanjo zilizotolewa wao wanasema inawezekana uliwahi kupata maambukizi ya Uviko bila kujua na ukapona pia bila kutumia dawa zozote.

Utajua hilo kama umewahi kuona ishara zifuatazo kwenye afya yako ambazo huka kwa kipindi kirefu hadi wiki mbili;

Asidi nyingi tumboni (GERD)
Pengine wakati wenzako wakisema wanaumwa vichwa na mafua wewe hukuwa na shida hiyo bali ulikuwa na gesi nyingi tumbonina kinywa kujaa mate.

Kupoteza fahamu
Pengine mara kadhaa ulisikia kizunguzungu cha ghafla kutokana na ufinyu wa damu inayoingia kwenye ubongo na kufanya upoteze fahamu kwa muda.

Kuongezeka kwa mba
Mba wa kichwa huweza pia kusababishwa na homoni kukosa urari na hivyo kusababisha ngozi ya kichwa kukauka ambapo moja kati ya athari za virusi hivyo ni pamoja na kuharibibu uwiano wa homoni mwilini.

UTI
Ugonjwa huu wa njia ya mkojo ni moja kati ya magonjwa ambayo badhi ya watu waliokuwa na Uviko walikutwa nao. Hopkins wanasema UTI inaweza kuwa ishara mojawapoya kuwa umepata mambukizi ya Uviko.

Midomo kubadilika rangi na kupasuka
Dalili nyingine ni midomo kubadilika rangi na kuanza kuwa kama zambarau kwa kukosekana kwa oksijeni ya kutosha kwenye damu vilevile kukosa maji ya kutosha mwilini kupelekea kupasuka kwa midomo.

Kunusa harufua ambazo hazipo kwenye mazingira yako (phantosmia)
Zinaweza kuwa ni harufu nzuri ama mbaya lakini ni harufu ambazo hazipo katika mazingira yanayokuzunguka kwa wakati huo.

error: Content is protected !!