Sera za Rais Samia zilivyoimarisha shilingi ya Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo

HomeKitaifa

Sera za Rais Samia zilivyoimarisha shilingi ya Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo

Tangu aingie madarakani Machi 19, 2021 , Rais Samia Suluhu ameweza kuimarisha thamani ya shilingi ya Tanzania na kuendelea kuwa imara ikilinganishwa na mwenendo wa thamani za shilingi za nchi jirani.

Kwa kuendelea kuimarika kwa shilingi ya Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo ni dhahiri kwamba Rais Samia anafanyia kazi ahadi yake ya kwamba ataendeleza kazi za watangulizi wake na kuhakikisha Tanzania inabaki salama huku ikipata maendeleo endelevu.

Sababu za kuimarika kwa shilingi ya Tanzania

Sera za kiuchumi zenye utulivu: Rais Samia amedumisha utulivu wa kiuchumi kwa kudhibiti matumizi ya serikali, kudumisha usawa katika biashara na uwekezaji, na kudhibiti mfumuko wa bei hatua ambazo zimechangia kuimarika kwa shilingi ya Tanzania.

Ukuaji wa uchumi: Kutokana na usimamizi bora wa sera za fedha chini ya Rais Samia uchumi wa Tanzania umezidi kukua na hivyo kupelekea kuendelea kuimarika kwa shilingi ya Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Amani na utulivu nchini: Kwa miaka mitatu mfululizo shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika kwa sababu Rais Samia ameendelea kudumisha amanai na utulivu nchini jambo lililoweza kuvutia zaidi wawekezaji na wafanyabiashara kuja kuwekeza nchini na kuongezeka kwa wawekezaji wazawa jambo ambalo limechangia kuimarika kwa shilingi ya Tanzania.

Aidha hatua anazochukua Rais Samia Suluhu katika kuhakikisha shilingi ya Tanzania inazidi kuimarika zimetambulika duniani na wengi wakimpongeza kwa mwenendo mzuri wa uchumi wa Tanzania.

Hali ya shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na nchi jirani

 

error: Content is protected !!