Zumaridi ahukumiwa mwaka mmoja jela

HomeKitaifa

Zumaridi ahukumiwa mwaka mmoja jela

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imemhukumu Diana Bundala maarufu ‘Mfalme Zumaridi’ kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kumkuta na hatia katika makosa mawili kati ya matatu kwenye kesi ya jinai namba 10/2022.

Akisoma hukumu hiyo leo Januari 25, 2023, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Monica Ndyekobora amesema Zumaridi na wenzake wanne wamekutwa na hatia katika makosa mawili ambayo ni pamoja na kumzuia Ofisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Nyamagana, Christina Mwisongo (46) kutekeleza wajibu wake na kuzuia maofisa wa polisi kutekeleza jukumu lao.

Pamoja na kosa hilo, Hakimu Ndyekobora amewakuta hawana hatia katika kosa la shambulio la kudhuru mwili.

Katika kesi hiyo, washitakiwa wengine wanne wameachiliwa huru.

Hata hivyo, Zumaridi atatumikia mwezi mmoja katika gereza la Butimba jijini Mwanza kutokana na kukaa miezi 11 mahabusu wakati kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa, huku wenzake wanne wakitumikia kufungo cha nje.

error: Content is protected !!