Dkt. Mpango aeleza sababu ya kifo cha Lowassa

HomeKitaifa

Dkt. Mpango aeleza sababu ya kifo cha Lowassa

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ametangaza kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa kilichotokea leo tarehe 10 Februari 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa hiyo Dkt. Mpango amesema, Mhe. Lowassa aliugua kwa muda mrefu tangu Januari 14,2022.

“Mhe. Lowassa amefariki leo tarehe 10 Februari, 2024 saa nane mchana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu kwa ugonjwa wa kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu.”- Dkt. Mpango

Dkt. Mpango amesema Hayati Lowassa ameugua kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu tangu Januari 14, 2022 katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na baadae akapelekwa kwa matibabu zaidi nchini Afrika Kusini na kurejea tena Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Aidha, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ametangaza siku tano za maombolezo bendera itapepea nusu mlingoti kuanzia leo tarehe 10 Februari 2024.

error: Content is protected !!