Rais Samia asisitiza ulindwaji wa amani na utulivu nchini

HomeKitaifa

Rais Samia asisitiza ulindwaji wa amani na utulivu nchini

Ikiwa jana Septemba 15,2023 ni siku ya Demokrasia Duniani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi na viongozi wa kisiasa mkoani Mtwara kutoharibu amani na utulivu uliopo kwa kutumia vibaya uhuru wa demokrasia .

Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mtwara jeo katika Viwanja vya Nangwanda Sijaona vilivyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani Rais Samia amesema kuwa yapo baadhi ya maeneo ndani ya Mkoa wa Mtwara viongozi wa siasa wanatumia demokrasia kufifisha maendeleo badala ya kuhamasisha maendeleo.

Ameongeza kwa kusema kuwa Serikali inapoleta fedha za maendeleo pamoja na demokrasia iliyopo kuwa wananchi wana haki ya kusema hili liende kule na hili lisiende kule.

Ameendelea kubainisha kuwa zinapoletwa fedha za maendeleo zikahudumie wananchi wenye mahitaji husika na sio kuchagua wanufaika kutokana na itikadi za kisiasa.

Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Mkoani Mtwara ilianza Septemba 14,2023 ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani na itamalizika Septemba 17 katika Wilaya ya Masasi.

error: Content is protected !!