Rais Samia: mbaazi ni zao la biashara

HomeKitaifa

Rais Samia: mbaazi ni zao la biashara

Rais Samia Suluhu Hassan amesimama kuwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Nanguruwe Mkoani Mtwara leo September 16,2023 ambapo amewataka Wakazi wa Mikoa ya Kusini kuondokana na dhana kuwa mbaazi ni mboga pekee na kuliona kwamba ni zao la biashara na kuwataka walime zao hilo kwa wingi kwakuwa soko lake ni la uhakika.

“Mbaazi sasa sio mboga ni zao la biashara kwahiyo wekeni jitihada kwenye kilimo kikubwa cha mbaazi soko lipo tumeshaweka mikataba na Nchi zinazonunua kwahiyo soko la uhakika lipo”

“Kama ilivyopanda bei mwaka huu bei zitaendelea kuwa hivyo kwahiyo kalimeni sana mbaazi, ufuta na korosho, jinsi tunavyoongeza thamani ya zao letu ndivyo bei zitakavyopanda”

Aidha, Rais Samia pia amewasihi wazazi kuhakikisha wanawapelekea watoto wa kike shule kwani serikali inajenga na inaendelea kujenga shule maalum kwa wanafuniz hao.

 

error: Content is protected !!