Ahadi ya Rais Samia kwa WaKenya

HomeKitaifa

Ahadi ya Rais Samia kwa WaKenya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amempongeza Rais wa Kenya William Ruto kwa kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa nchi hiyo lakini pia kuwapongeza wananchi wa Kenya kwa kufanya uchaguzi wa haki na amani.

Akizungumza kwenye hafla ya uapisho iliyofanyika Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi, Rais Samia alisema zawadi kubwa waliotoa wananchi wa Kenya kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni zawadi ya amani waliyoiweka kipindi cha uchaguzi.

“Nataka niwaambie ndugu zetu Wakenya, kama kuna zawadi mliyoitoa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka huu ni zawadi ya amani mliyoiweka katika uchaguzi. Tunawashukuru sana kwa zawadi hiyo muhimu.” amesema Rais Samia.

Pia amewahakikishia wananchi wa Kenya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ili kuleta maendeleo yatakayo nufaisha mataisha yote.

“Nitumie fursa hii kuhihakikishia Kenya dhamira yetu ya dhati ya kufanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu zaidi katika kuleta maendeleo ya pamoja ya kijamii na kiuchumi baina ya nchi zetu lakini na ukanda wote wa Afrika Mashariki.”amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!