Mama apambana na Simba kumuokoa mwanae.

HomeKimataifa

Mama apambana na Simba kumuokoa mwanae.

Mwanamke mmoja amnusuru mwanae wa miaka mitano kuwa mlo wa Simba huko California nchini Marekani.

Mtoto wa miaka mitano alishambuliwa na Simba wa milimani huko Calabasas katika milima ya Santa Monica, Magharibi mwa Los Angeles.Simba alifanikiwa kumburuza mtoto huyo kwenye nyasi lakini Mama yake bila woga alikimbia na kumpiga Simba kwa mikono yake hadi kumuachia mtoto wake.

Simba huyo alipatikana baada ya kupigwa risasi na Mamlaka ya wanyama pori.

Mtoto amepata majeraha kichwani na mwilini, kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari kwa matibabu zaidi.Mamlaka ya wanyama pori imesema kuwa Simba huyo alikua mchanga anayejifunza kuwinda.

error: Content is protected !!