Ijue nyota yako leo Septemba 13, 2021

HomeNyota

Ijue nyota yako leo Septemba 13, 2021

MBUZI (Dis 22 – Jan 20): Ni siku yako ya mafanikio, ni kipindi cha majadiliano na wengine, bila ya kujali tofauti zilizopo Kuwa mwenye zaidi kusikiliza mambo kuliko kuwa msemaji, hali ambayo itawavutia wengi kuvutiwa na mchanganuo wa mawazo yako. Unaonekana ubora wako katika jamii, cha msingi ni kuhakikisha kwamba jarnii inakufahamu na kuelewa mchakato wa mambo yaendavyo kwako.

NDOO (Jan 21 – Febr 19): Mawazo yako, uwezo uliokuwa nao kiujumla katika kushawishi na jinsi unavyozungumza utavutiwa na wengi. Ni kipindi cha kutoa maamuzi kwani mambo mengi uliyopanga yatakwamuka. Hutarudi nyuma na furaha itatawala kwa maamuzi yako hasa kuhusiana na mambo uliyokuwa na wasiwasi nayo hapo kabla. Tumia muda mwingi kuwa karibu na familia yako.

SAMAKI (Feb 20 – Machi 20): Muda wa upinzani unakaribia kwako. Haijalishi kama una mapenzi katika michezo au masuala ya utaalamu ikiwemo alira. Upinzani utajitokeza katika sehemu kubwa ya masuala yaliyokuzunguka. Unahitaji ushindi, lakini kuna changamoto nyingi zinajitokeza katika kufikia lengo lililokusudiwa. Kuwa mwangalifu katika kukwamua mambo yako ya msingi.

KONDOO (Machi 21 – April 20): Chukua mapumziko ya muda mfupi na waache wengine washughulike kwa niaba yako katika masuala yaliyokuhusu. Wakati huo huo waweza kugundua nyingi mbadala ambazo zitakusisimua na kuchukua sehemu kubwa ya muda wako kwa mapumziko. Hutakuwa na uchovu baada ya mapumziko ya kutosha kutokana na wingi wa mambo yalivyokuzonga. Jenga tabia ya kuwa karibu zaidi na rafiki zako wa karibu.

NG’OMBE (April 21 – Mei 21): Ni siku maalum na njema kwako kuwa karibu na watu unaowajali zaidi. Licha ya kuwa ni mwenye kuwajibika zaidi na masuala ya kijamii katika kipindi cha hivi karibuni, pia umekuwa ni mwenye wingi wa furaha kutokana na mambo yako mengi kuweza kukamilika kama ulivyopanga. Kuwa karibu na marafiki ambao watatoa mchango mkubwa katika mafanikio yako. Kuwa mwangalifu zaidi.

MAPACHA (Mei 22 – Juni 21): Hamu yako sasa ni kuwa huru. Hakuna jambo lolote kubwa zaidi ya kutaka kushangaza wengine katika kufanikisha masuala yako ya msingi. Mpango wako wa kuelekea katika eneo jiengine la kazi ulilokuwa ukilitarajia kwa muda mrefu litakamilika. Jiandae na mambo yako ya msingi yajayo na achana na tabia ya kukurupuka hasa katika kutoa maamuzi ya haraka.

KAA (Juni 22 – Julai 22): Utakuwa ni mwenye kufuatiliwa na wengi katika siku za hivi karibuni. Hawatafanikiwa kwa walilokuandalia ambalo yapenekana kuwa linaweza kuwa na athari baadae. Licha ya kwamba umeshalifanyia mazoezi ya uhakika jambo hilo bado linapenekana kuwa na mashaka kuweza kukamilika kwa wakati. Hatimaye utagundua utata kwa mengi ya yaliyokutatiza. Hii ni faraja kubwa kwako.

SIMBA (Julai 23 – Aug 23): Ijapokuwa maamuzi yako sio sahihi, pia utajuta kwa kugundua kuwa hutaweza kukamilisha mambo yako mengi kwa wakati uliopanga. Kuwa na msimamo imara ni sehemu ya mafanikio. Yaonekana kuwa na mambo mengi uliyoyaandaa kwa uhakika hapo kabla. Hii itapelekea kuondokana kwa haraka kwa shida nyingi zilizokuwa zikikutatiza kabla.

MASHUKE (Aug 24 – Sept 23): Inapotokezea wakati wa kutatua matatizo mengi ya msingi, jitahidi kufanya hivyo ukizingatia kuwa wingi wa matatizo hayo yamekuwa yakikusumbua kwa muda mrefu sasa. Licha ya kwamba uko vyema katika kushughulikia mambo mengi sio tu yanayokwamisha mipango ya maisha yako bali pia mpenzi wako pamoja na marafiki. Watu wanapenda kuwa nawe karibu hasa kwa jinsi unavyowapa matumaini pamoja na kuwajali.

MIZANI (Sept 24-Okt 23): Ni kipindi cha mafanikio makubwa katika sehemu yako ya kazi. Kila ulilokuwa ukilitarajia kwa muda mrefu litazaa matunda ya mafaniko. Ni wakati wa kujiimarisha kimaisha. Kusaidia wengine ni jambo la msingi, jenga utamaduni wa kusaidia kila inapobidi. Hatua hii itasaidia kukwamua wingi wa changamoto. Watu watakaokuwa wakidhani una matatizo hapo kabla watakuelewa na watakuwa pamoja nawe.

NGE (Okt. 24 – Nov. 22): Hofu yako sasa imekuelekeza katika kiwango mafanikio. Utagundua ni vigumu kuwafahamu wengine ambao mara nyingi hufanya mambo bila ya utulivu ama ukamilifu na utapendelea Zaidi kushughulikia wenye kufanana na tabia nawe. Jitahidi kupanga mipango yako ya muda mfupi ambayo utaweza kuitekeleza kwa wakati, kuliko kuwa na wingi wa mipango ya muda mrefu ambayo kukamilika kwake haitakuwa rahisi

MSHALE (Nov. 23-Dis. 21): Sasa umeshakusanya maoni kutoka sehemu tofauti. Hilitatoa hofu kutoka kwa wengine ambao umetumia muda mwingi kuwa karibu nao na kufanya shughuli za pamoja. Tatizo kubwa ni kwamba kile unachokiamini leo ni tofauti na kile cha jana. Hali hii huweka wakati mgumu kwa wengine kuweza kuungana nawe. Jaribu kuwa na mwendelezo kila inapowezekana.

error: Content is protected !!