Ifahamu safari ya kundi la Taliban kutoka msituni hadi Ikulu.

HomeKitaifa

Ifahamu safari ya kundi la Taliban kutoka msituni hadi Ikulu.

Tangu kundi la Taliban litwae utawala wa nchi ya Afghanistan kumekuwa na habari na taarifa nyingi kuhusu kundi hilo. Lakini umewahi kuwa nini hasa chimbuko la kundi hilo. Fuatana nami hapa kufahamu chimbuko la kundi la Taliban ambalo linaweza kuhusishwa na mambo mengi sana, lakini tutaangazia kwa ufupi namna lilivyoanza na lengo lake hasa hadi kufikia wakati huu.

Mwaka 1973, Mohammed Daoud Khan, kiongozi mwenye sera za kijamaa (Communist) aliingia madarakani nchini Afghanistan. Daoud aliishikamanisha nchi hiyo na Taifa la Urusi (wakati huo ikiwa kwenye muungano wa USSR). Kabila la Pashtu la nchini Afghanistan lilichukizwa na kitendo hicho na kuona kwamba wanaipoteza nchi yao, ndipo wakaingia msituni ili kuikomboa’ nchi yao.

Mapigano dhidi ya Urusi yaliendelea hadi walipoondoka mwaka 1989, na mwaka huo vita vya wenyewe kwa wenye vilivyosimama kwa miaka 10 ili kumfukuza Mrusi nchini Afghanistan, vikarejea tena.

Kundi la Taliban likaanzishwa rasmi mwaka 1994 na watu wawili, Mullah Omar na Mullah Abdul Ghani Baradar likiwa na lengo kubwa la kuigeuza Afghanistan kuwa nchi inayofuata sheria ya Kiislam.

Lengo lao lilifanikiwa na wakatwaa madaraka mwaka 1996 na kuiongoza nchi hiyo chini ya “sharia” hadi mwaka 2001. Katika miaka mitano ya utawala wa Taliban chini ya Mullah Omar, mataifa matatu tu duniani ndiyo yaliitambua nchi hiyo ambayo ni Saudi Arabia, Pakistan na Umoja Falme za Kiarabu, nchi ambazo zinahusishwa kwa namna fulani na mapigano ya Afghanistan.

Mwaka 2001 wakati Marekani na Umoja wa Mataifa walipovamia nchi hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kurejesha demokrasia, Taliban walikimbilia mwituni kupambana, na inadaiwa kuwa walipata ufadhili kutoka kwa Saudi Arabia.

Mgogoro wa Taliban na Marekani uliendelea kwa kipindi chote na itakumbukwa mwaka 2010, kiongozi namba mbili wa Taliban, Mullah Abdul Ghani Baradar alikamatwa na kuweka gerezani nchini humo, na mwaka 2013, kiongozi namba moja Mullah Mohammad Omar alifariki Dunia (ilifanywa siri hadi mwaka 2015).

Mambo yalibadilika na kuchukua sura mpya wakati Rais Donald Trump alipoingia madarakani mwaka 2016 nchini Marekani. Miaka miwili baadaye alimwachia huru Baradar ambaye alikamatwa wakati wa utawala wa Rais Barack Obama.

Ukaribu wao ulidhihirika tena alipotaka kumwalilka Baradar kwenye kambi ya kijeshi ya Marekani, Camp David, Septemba 11, 2019. Hakuishia hapo, mwaka 2020 aliliondolea vikwazo kundi hilo na kuwaachia huru wanamgambo 5,000 kutoka gerezani. Miaka minne baada ya kuachiwa huru na Rais Trump, sasa Baradar ndiye anaiongoza Afghanistan kupitia kundi la Taliban.

error: Content is protected !!