Taliban yaunda serikali ya mpito

HomeUncategorized

Taliban yaunda serikali ya mpito

Kikosi cha Taliban kimetangaza kuunda serikali ya mpito nchini Afghanistani ambapo wameweka bayana kuwa serikali hiyo itaongozwa na moja ya viongozi waanzilishi wa kundi hilo, Mulla Mohammad Hassan Akhund na makamu wake atakuwa Ghani Baradar.

Kiongozi mwingine muhimu aliyeteuliwa kuunda serikali ni Sarajuddin Haqqani ambaye atakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Haqani anaongoza mtandao wa siri wa kijeshi uitwao ‘Haqqani Network’ ambao una ukaribu sana na kundi la Taliban. Taliban na Haqqani network walishirikiana sana kufanya mashambulizi ya hatari katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Makerani imesema kuwa Haqqani Network ni kundi la kigaidi linalofanya kazi kimataifa.

Viongozi wengine waliopata uteuzi ni Mullah Yaqoob kama Waziri wa Ulinzi, Amir Khan Muttaqi Waziri wa Mambo ya Nje na Mullah Abdul Salam Hanafi kama Naibu Waziri wa Mambo ya Nje.

error: Content is protected !!