Ruto aitaja SGR ya Tanzania mfano bora wa uwekezaji wa kikanda

HomeKimataifa

Ruto aitaja SGR ya Tanzania mfano bora wa uwekezaji wa kikanda

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. William Samoei Ruto, ameipongeza Tanzania kwa mafanikio ya mradi wa reli ya kisasa (Standard Gauge Railway (SGR)

Akizungumza katika Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha, Rais Ruto, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo aliyemaliza muda wake, amesema mradi huo ni muhimu katika kuimarisha muunganiko wa miundombinu na kukuza uchumi wa ukanda wa Afrika Mashariki, sambamba na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo na abiria.

“SGR ya Tanzania inayosafirisha wastani wa abiria 10,000 kwa siku kati ya Dar es Salaam na Dodoma ni hatua kubwa ya kuimarisha muunganiko na maendeleo ya ukanda wa Afrika Mashariki,” alisema Rais Ruto.

error: Content is protected !!