EWURA yatangaza ongezeko la bei za mafuta

HomeKitaifa

EWURA yatangaza ongezeko la bei za mafuta

Bei za mafuta nchini zimeongezeka kwa zaidi ya shilingi 200 kwa lita, kuanzia leo Oktoba 7, 2026. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Dar es Salaam, petroli itauzwa kwa Sh4,057 kwa lita kutoka Sh3,796 mwezi Septemba, huku dizeli ikipanda hadi Sh4,086 kutoka Sh3,877. Mafuta ya taa yameongoza kwa ongezeko, yakipanda hadi Sh4,067 kutoka Sh3,713 kwa lita.

EWURA imesema ongezeko hilo limetokana na kuendelea kwa migogoro Mashariki ya Kati, ambayo imeathiri uzalishaji, upatikanaji na usafirishaji wa mafuta duniani.

Serikali imesema inaendelea kufuatilia hali ya soko la mafuta duniani na kuchukua hatua kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini unaendelea kuwa wa uhakika.

error: Content is protected !!