Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika kipindi cha miezi sita, idadi kubwa ya wawekezaji wamejitokeza kuwekeza Tanzania katika sekta mbalimbali, ambapo mmojawapo ni ujenzi wa kiwanda cha mbolea ambacho kinaendelea kujengwa Dodoma.
Rais Samia aliyasema hayo jana jijini Dodoma alipowasili akitokea Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja tangu aliporejea nchini kutokea New York, Marekani alikohutubia Mkutano Mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa (UN), Septemba 23, mwaka huu.
“Kwa ujumla mambo yetu si mabaya, ni mazuri. Ulimwengu upo tayari kufanya kazi nasi, yale yaliyosemwa hapa ya umeme, maji madarasa na mambo mengine, nataka niwahakikishie wana Dodoma hiyo kero tunakwenda kumaliza,” alisema.