Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri amesema wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Wamachinga wanaokaidi agizo la kutofanya biashara katika maeneo waliyozuiliwa watashitakiwa mahakamani huku akihimiza wananchi watoe ushirikiano kuwabaini wale waliorudi kinyemelea kwenye maeneo hayo baada ya kuondolewa.
“Tunaendeela na operesheni katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha tunawakamata na kuwafikisha mahakamani, kikubwa naomba wananchi wote kuendelea kutupa ushirikiano ili tuweze kufanikisha dhumuni la kuwaondoa,” alisema Shauri.
Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamachinga Tanzania, Stephen Lusindeamesema suluhisho la kuimaliza changamoto hiyo ni kwa serikali kukaa nao wazungumze.
“Tunashukuru serikali kwa kuainisha maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia machinga kufanya shughuli zao, kikubwa tunazidi kuiomba kutupatia maeneo mengi mazuri yenye nafasi ya kutosha kutuwezesha kufanya shughuli zetu,” alisema Lusinde.