Kampuni ya Apple kuacha kuzalisha iPhone 13 kwa muda kutokana na uhaba wa vipuli (spare) aina ya ‘chip’, kipuli ambacho hufanya simu za iphone kufanya kazi kwa kasi na ufanisi.
Mwaka 2021 iPhone itapunguza uzalishaji wa simu zaidi ya milioni 10 kutokana na uhaba wa kipuli hicho muhimu. Apple ndani ya miezi mitatu iliyopita ilipanga kuzalisha iPhone tofauti milioni 90, lakini idadi hiyo itapungua zaidi kutokana na uhaba wa vipuli.
Kampuni ya Apple imekuwa ikinunua vipuli kutoka kampuni kama Broadcom Inc na Texas Instruments. Apple hununua vioo vya simu zake kutoka Texas Instruments and hutumia vifaa vya ‘Wireless’ kutoka kampuni ya Broadcom Inc. Na kwa sasa inapitia wakati mgumu wa kupata vipuli kutokana na wasambazaji wake kupunguza uzalishaji.
Tangu tangazo hilo litoke hisa za Apple zimeshuka kwa asilimia 1.6. Wakati fulani mwaka 2021 hisa za Apple zilikuwa juu kwa 6.6%. Hadi hivi sasa Apple inapitia kipindi kigumu kupitia usambazaji wa simu zake kushuka, na kwa kipindi cha mwezi mmoja Apple haitouza simu zake kwa njia ya tovuti yake.
iPhone 13, iPhone 13 Pro na iPhone 13 Pro Max hazitopatikana kwa sasa hadi kuanzia katikati ya Novemba, na nyingine kuanza zitaanza kupatikana kuanzia mwezi wa 12 kutokana na sikukuu ya Krismasi. #clickhabari