Biashara 12 zinazolipa, zinazohitaji mtaji chini ya TZS Laki 1

HomeBiashara

Biashara 12 zinazolipa, zinazohitaji mtaji chini ya TZS Laki 1

 Sio sawa kusema kuwa kuna biashara ndogo, bali unaweza kufanya biashara kwa mtaji mdogo. Matendo yetu huongozwa kwa mawazo na fikra zetu, hivyo kuanza kusema biashara ndogo inaweza kuathiri muonekano wa biashara yako na hatimaye kushusha ari ya kupambana kufika pakubwa zaidi.

Sio kila biashara inahitaji mtaji mkubwa kuazisha, zipo biashara zenye mtaji mdogo lakini matokeo yake ni makubwa. Kukosa mtaji ni moja ya kikwazo cha kuanzisha biashara, lakini kikwazo kikubwa zaidi ni kukosa mawazo sahihi juu ya biashara unayotaka kufanya. Hizi hapa biashara 15 zenye mtaji chini ya 100,000 ambazo zina matokeo makubwa.

  1. Kupika kwa Oda
    Kama wewe ni mpishi mzuri au una mtu unaamini anajua kupika vizuri, basi fanya jitihada ya kujitangaza kwenye ofisi na watu mbalimbali katika mazingira yako. Chukua oda za watu wachache wapikie halafu subiria majibu yao. Jiboreshe kulingana na maoni yao na kila chakula chako kikizidi kuwa kizuri na kupendwa basi itakuelea wateja wengi zaidi na biashara yako itakuwa zaidi. Lakini, hakikisha unakuwa mbunifu zaidi.
  2. Urembo (Kusuka, Makeup, Kucha)
    Urembo ni moja huduma ya gharama sana kwa wasichana, licha ya gharama zake lakini wasichana/wanawake huwaambii kitu kuhusu kuwa na muonekano wa kuvutia muda wote. Basi hapo mtaani kwenu hutokosa wateja wa kusuka, kusafisha kucha au hata kupaka make up. Ifanye ndio biashara yako na itangaze hatimaye itakuwa huitaji fedha nyingi kabisa kuanza biashara hii.
  3. Kilimo cha Mbogamboga
    Biashara hii huitaji mtaji mkubwa wala eneo kubwa kufanya. Unaweza kuwa na eneo dogo tu lakini likakuleta matokeo makubwa hadi ukashangaa. Tumia kama Youtube kujifunza namna gani unaweza kuandaa eneo dogo liweze kukuletea matokeo mazuri kwenye biashara. Unaweza kuanzisha kilimo cha mbogamboga hata kwenye mifuko ya sandarusi (sulphate) au madebe ya maji kwa kuyajaza mchanga ambao una mbolea vizuri.
  4. Kupiga Picha
    Kununua Kamera yenye viwango vizuri ni gharama sana, lakini Kamera hizohizo hukodishwa kati ya shilingi 20000 hadi 30000 kwa siku. Kufanya kazi ya kupiga picha kwenye shughuli kama harusi inaweza kukuingizia hadi 300,000 kwa shughuli moja tu. Kama huna ujuzi wa kupiga picha basi hujachelewa kujifunza kupitia mitandao. Kikubwa uwe na moyo wa kujifunza na kupenda unachokifanya.
  1. Kupanga Sherehe/Matukio (Event Planning)
    Biashara hii inataka sana uwe mtu wa kujichanganya sana na watu na uwe na wigo mkubwa wa kujua watu wengi. Hiki ni kipawa ambacho huitaji fedha kuwa nacho, ni namna gani tu umechangamka. Kuanzia harusi, sendoff, kitchen party na sherehe nyingine katika ngazi ya jamii, unaweza kuwa ndio kinara wa kuhakikisha zinakwenda vizuri kabisa. Kazi yako ni kuumizwa kichwa kutafuta watu na huduma mbalimbali kama vile wapambaji, ma dj, au kuwatafutia usafiri na kutafuta watu wa chakula.
  2. Kutembeza Watalii (Tour Guide)
    Biashara hii inategemea na eneo unaloishi. Katika mikoa kama Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Dar es Salaam na hata Zanzibar vijana wengi wanajihusisha na shughuli hii kulingana na mazingira yao. Unaweza kutumia simu yako kupiga picha vivutio katika eneo lako, ukaweka mtandaoni kupitia kurasa zako za mitandao ya kijamii na zikakusaidia kukuletea wateja. Sio lazima wawe wazungu, bali hata watu wa kawaida tu wanaweza kupenda na kutembelea eneo lako.
            > Hii ndiyo sababu ya kupanda kwa bei ya nyama
  3. Ushonaji Nguo
    Ushonaji ni moja ya biashara inayokuwa kwa kasi sana nchini Tanzania kwa sasa. Watu wengi wameanza kuwa na muamka wa kupenda sana kuvaa nguo za kushona kuliko nguo za viwandani kutoka nje. Hii inaweza kuwa fursa kwako. Ni swala la kujifunza tu, lakini kabla hujafanya hvyo hakikisha una mapenzi na kitu hiki ili kuepusha kukata tamaa na kupoteza muda mapema. Njia za kujifuza ziko nyingi, ukitoa mitandao ya kijamii, unaweza kuenda kwa mtu mzoefu wa kazi hiyo na kuongea nae mkakubaliana namna ya kukufundisha kazi hiyo, lazima mwisho wa siku kutakuwa na makubaliano baina yetu namna ya kufanya kazi pamoja.
  4. Kufundisha (Tuition)
    Vijana wengi waliotoka vyuo vikuu wengi wako tu mitaani na wengine hawajui waanzie wapi au wafanye nini. Lakini kupitia elimu ambazo wanazo, wanaweza kuanzisha sehemu za kufundisha wanafunzi wa shule za sekondari na za msingi na kujiingizia kipato. Cha kufanya ni kuanza kujitathmini na kujua ubora wako uko sehemu gani katika masomo, halafu anzisha darasa kwa vijana au watoto walioko katika mazingira yako.
  5. Biashara ya Saluni ya Kiume
    Hii pia ni biashara isiyokuwa na msimu kwavile nywele huota kila siku. Jifunze kunyoa watu nywele halafu anza na wale wakaribu yako kama vile marafiki na ndugu. Utakapofanya kazi nzuri hao watakuwa wateja wako wakujirudia na pia kukutangazia huduma zako kwa watu wengine. Unachohitaji ni kununua mashine ya kunyolea ambayo unaweza kupata kwa chini ya elfu hamsini. Anza kununua kwa mtu (used), na baada ya muda utaweza kununua mpya.
  1. Kuuza miti ya Maua
    Maua hupendezesha nyumba na wengi huamua kupanda nyumbani kwao. Fuatilia jinsi gani maua tofauti yanavyopandwa na kisha yapande. Kwa wastani, mti mmoja wa maua huuzwa kuanzia elfu mbili. Mtaji mkubwa hapa ni muda wa kupanda na kuishughulikia hiyo miti.
  1. Kufulia watu nguo majumbani
    Watu wengi leo hii wametingwa na kazi nyingi kiasi kwamba wanakosa kabisa muda wa kufua nguo zao wenyewe. Hivyo hupendelea kuwapa kazi watu wengine wawafanyie kazi hizo wao wakiendelea na shughuli nyingine. Kwa majiji makubwa ni vyema kuanza kutembelea nyumba za watu, ukiwa umevaa vizuri na pia uweze kujielezea vizuri unafanya nini na kwanini. Ukiweza kujielezea ni rahisi sana mtu kukuelewa hata kukuamini na kukupa kazi ya kufanya. Unaweza ukatumia hela ukawa na sabuni zako, au watu wengine unakuta wana sabuni zao pendwa tayari kwa kufulia nguo zao.
  2. Kuuza Vocha za simu
    Kuna maeneo bado huduma za kurusha fedha kwa simu ni adimu au ziko mbali. Hivyo kuwa na vocha za elfu hamsini kibindoni zinaweza kusaidia watu wasitembee umbali mrefu kufuata vocha. Cha kufanya ni kusoma mazingira yako na kujua shida iko sehemu gani ili uweze kufanya maamuzi kulingana na mtaji na biashara yako.
error: Content is protected !!