Kutokana na hali ya baridi watu wengi wanasumbuliwa na mafua, mafua ambayo yanaambatana na maumivu ya mwili, kuhisi baridi, homa, kuhisi mwili mzito pamoja na pua kubana. Unaweza kutumia dawa za asili za nyumbani kutibu mafua hayo.
1. Tangawizi
Chukua kipande cha tangawizi kisha kioshe. Menya maganda na utafune, kutokana na ukali wake unaweza kuisaga kisha tia kwenye sufuria na maji kidogo, chemsha. Ikishachemka ipua na unywe ikiwa ya vuguvugu.
2. Asali
Asali ina uwezo mkubwa wa kukabiliana na vijidudu katika mwili na kufanya kazi kama “antibiotics” hivyo kupunguza koo kuwasha na kutibu kifua, chukua asali changanya na chai na tia na kipande cha limau na unywe.
3.Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu kinasaidia katika kupabana na maambukizi mafua na ili kuweza kuapata matokeo unaweza kunywa juisi ya vitunguu swaumu au ukatafuna. Chukua vitunguu swaumu kiasi viponde halafu uvimumunye vikiwa vibichi kwa muda wa dakika 15. Lakini pia unaweza kuchanganya vitunguu swaumu vilivyoponda na asali na kunywa chai yake.
4. Maji ya chumvi
Chemsha maji yao kikombe kimoja cha chai yakisha pata moto chukua chumvi nusu kijiko cha chakula na uchanganye, wakati wa kunywa maji hayo usimeze haraka haraka yaache kwa muda kooni ili usafishe koo lako.
Pamoja na dawa hizi za asilia ambazo unaweza kutumia nyumbani ambazo hazina madhara lakini pia ni muhimu kwenda kituo cha afya endapo utaona una mafua na kifua ambacho hakiponi kwa muda. Pia inabidi uzingatie kunywa maji mengi katika kipindi hicho cha kuumwa mafua na kifua.