Rushwa yanuka TARURA, Afisa Ugavi abanwa na TAKUKURU

HomeKitaifa

Rushwa yanuka TARURA, Afisa Ugavi abanwa na TAKUKURU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohammed Mchengerwa ametoa agizo la kusimamishwa kazi kwa Afisa Ugavi Mkuu TARURA kufuatia ufisadi katika miradi ya TARURA.

Agizo hilo lilitolewa majuzi ya Waziri Mchengezwa na kuielekeza mamlaka ya kupambana na kudhibiti rushwa TAKUKURU kuchunguza mikataba yote ili kubaini ufisadi kisha kuchukua hatua za kisheria.

Wakati uchunguzi unaendelea, Afisa Ugavi aliyesimamishwa kazi atahitajika kuripoti katika ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora siku ya Jumatatu (leo) na nafasi yake itakaimiwa na mtu mwingine. Mchingerwa alitoa agizo hilo mkoani Kagera.

error: Content is protected !!