Tetesi za soka Ulaya leo Oktoba 02 (Henry akosoa kauli ya Wenger, Sterling njia panda Man City)

HomeMichezo

Tetesi za soka Ulaya leo Oktoba 02 (Henry akosoa kauli ya Wenger, Sterling njia panda Man City)

Mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia Dusan Vlahovic, 21, ana ndoto za kuhamia Manchester City. Mabingwa hao pia walihusishwa na uhamisho msimu huu (Gazzetta dello Sport).

Axel Tuanzebe, 23, yupo tayari kufanya mkopo wake kwa Aston Villa kutoka Manchester United kuwa mkataba wa kudumu (Birmingham Mail).

Raheem Sterling (26) bado anakabiliwa na sintofahamu kati yake na klabu yake ya Manchester City licha ya “kutokuwa na mahusiano mazuri” na Kocha Pep Guardiola (Daily Telegraph).

> Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 01 (Werner kurudi Bundersliga, Hatma ya Koeman Barcelona kuwekwa wazi Jumamosi hii)

Thierry Henry amekosoa mpango wa bosi wake wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger kuwepo na mashindano ya Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili, akiita “kuchosha akili” (Sun)

Manchester City waafikiria kutuma ofa ya kumsajili beki wa Villarreal na Uhispania Pau Torres, mwenye umri wa miaka 24 (Marca – Spanish).

Kocha wa Manchester Ole Gunnar Solskjaer amemwambia winga wa England Jadon Sancho (21) kuwa mvumilivu na kujituma, wakati akisubiri bao lake la kwanza katika klabu hiyo (Mirror).

Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 25, anakabiliwa na kupigania mustakabali wake klabuni hapo tangu kuwasili kwa Romelu Lukaku (London Evening Standard).

Real Madrid itakuwa na pesa ya kuidhinisha kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Haaland (21) msimu ujao, wakati huo wakimfuatilia kwa karibu nyota wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 22 (AS – Spanish).

Arsenal wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Italia Lorenzo Insigne (30) iwapo mchezaji huyo atakubali ataondoka katika klabu yake ya utotoni (Corriere dello).

Everton ipo mbioni kufanya uhamisho wa Januari kwa kiungo wa Newcastle Sean Longstaff, 23. (Independent).

error: Content is protected !!