Upinzani wamkubali Rais Samia

HomeKitaifa

Upinzani wamkubali Rais Samia

Doyo Hassani Doyo ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Alliance Democratic Change Tifa (CDC), amesema Rais Samia Suluhu ni kiongozi shupavu , mvumilivu kwani ameweza vyema ameendeleza tunu ya umoja na amani na kuiwezesha Nchi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika nyanja mbalimbali.

“Kama kiongozi wa kisiasa ninampongeza Rais Samia kwa hatua ambazo amechukua tokea kuwa Rais katika kipindi hiki kubwa kwa kuwa mvumilivu na shupavu kwa sababu kuwa Rais sio nafasi ndogo na hatujawahi kuwa na Rais Mwanamke kwenye Taifa letu.” alisema.

“Lakini pia mtazamo wangu, Rais Samia Suluhu kama Rais mwelekeo wa kisisasa unaleta matumaini makubwa sana nchini na sioni kama kuna tatizo, kwani hata nchi ambazo zimeendelea kama Marekani, Denmark na Sweden baada ya uchaguzi chama kilichopewa dhamana na wananchi kinafanya shughuli za maendeleo na siasa inakuja wakati wa uchaguzi.” Alisisitiza Katibu huyo.

Doyo alisema kuwa hata aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano, Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli, alitumia majukwaa kuhimiza maendeleo na kujenga heshima kwenye nchi na hivyo kwa mtazamo wake anaona hakuna tatizo kwenye upande wa siasa hapa nchini.

error: Content is protected !!