Sababu kama Afrika kutokuwa na majiji makubwa yaliyo bize, sababu za vinasaba (genetic) na historia ya kukumbwa na magonjwa makubwa mara kwa mara kama Malaria, Ukimwi, Polia na Ebola inaweza kuwa sababu ya bara la Afrika kutopota madhara makubwa ya virusi vya korona kinyume na ilivyo tarajiwa.
Ugonjwa huu ulipolipuka kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan nchini China mwaka 2019, hofu ya watu wengi ilikuwa ni ni je, itakuwaje ugonjwa huu ukifika barani Afrika ambapo huduma za afya na miundombinu mengine muhimu ya kukabiliana na dharura za kifya kama hii bado kuwa changamoto kubwa barani Afrika.
Licha ya Afrika kutokuwa na miundombinu muhimu pamoja na wataalamu wengi kwenye sekta ya afya ukilinganisha na mataifa mengine duniani, lakini madhara ya UVIKO-19 barani Afrika si makubwa kama ilivyo kwa mataifa mengine. “Afrika haina chanjo wala rasilimali muhimu za kupambana na UVIKO-19 kama ilivyo kwa Ulaya na Marekani, lakini Afrika inaonekana kufanya vyema zaidi kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huu” alisema Wafaa El-Sadr ambaye ni Mkuu wa Shirika la Global Health kutoka Colombia University.
Ripoti za Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa likiitaja Afrika kama bara liliodhaifu sana kwenye kupata maambuzi ya haraka ya magonjwa mbalimbali, lakini kwa hili la UVIKO-19, wataalamu wengi wamebaki vinywa wazi hata wasijue cha kusema kuhusu tukio hili.
Katika utafutaji wa majibu ya ajabu hiyo, wanasayansi wamekuja na majibu ya dhahania kwamba, pengine idadi kubwa ya bara la Afrika kuwa ni vijana inaweza kuwa sababu. Wanasayansi wanasema kuwa wastani wa mwaka barani Afrika ni 20 huku Ulaya ikiwa ni 43, hata hivyo pia Barani Afrika kutokana na hali za maisha ya uchumi, watu wengi hawatembei kutoka sehemu nyingine ukinganisha na ulaya, hivyo kupunguza uwezo wa kusambaza ugonjwa huo, huku wengine wakija na hoja ya vinasaba na historia ya bara la Afrika kukumbwa na magonjwa hatari zaidi, hali iliyowajengea uimara dhidi ya magonjwa mengine.
> Fahamu kirusi kipaya cha Corona aina ya Omicron
> Utafiti: Namna Vitamin C inavyoweza kutibu tatizo la UVIKO-19
Devi Sridhar, Mwenyekiti wa Global Public Health katika Chuo Kikuu cha Edinburgh anasema kuwa, “Afrika inautamaduni wa kupokea mambo tofauti ukilinganisha na mabara mengine, nadhani Afrika imepokea ugonjwa huu kwa busara wakiwa na imani kubwa, uvumilivu bila woga kwani tayari walishapata makubwa zaidi kama Ebola, Malaria na Polio”..
Afrika Kusini ndio nchi yenye rekodi ya vifo vingi barani Afrika, hadi Novemba mwaka huu watu 89,000 waliporipotiwa kufariki, huku takwimu za dunia kutoka Shirika la Afrika Duniani (WHO) zinasema kuwa vifo vyote duniani Afrika ni 3%, Marekani 46% na Ulaya 29%.
Nigeria, Taifa lenye watu zaidi ya 200 barani Afrika, Serikali imerekodi vifo 3000 pekee, ambapo idadi hiyo ni sawa na vifo vinavyorekodiwa Marekani kila baada ya siku 2 hadi 3.
“Walisema kuwa, miili barani Afrika itazagaa barabarani kutokana na ugonjwa huu, lakini kitu kama hicho hakijatokea”.. anasema kijana wa umri wa miaka 23 kutoka Nigeria Opemipo Are
Oyewale Tomori, mtaalamu wa virusi kutoka Nigeria ambaye mara kadhaa kupata fursa ya kuketi kwa majadiliano na wataalamu wa WHO, anasema kuwa pengine Afrika haiihitaji chanjo nyingi kama ilivyo kwa mataifa ya Ulaya.
Jarida la “American Journal of Tropical Medicine and Hygiene” lililochapishwa June 1, 2021 limeanisha sababu kadhaa zinazopelekea madhara na vifo kidogo barani Afrika kama vile, Hali ya hewa, idadi kubwa ya vijana, historia ya kukutana na magonjwa mengine, njia nzuri za kupambana na ugonjwa huo.
Ingawa kuna usambazwaji mdogo wa chanjo barani Afrika, lakini bado madhara ya UVIKO-19 sio makubwa ikilinganishwa na mabara mengine. Wapo wanaosema kuwa kwakuwa Afrika utunzaji wa data sio mzuri, pengine vifo vingi hutokea bila kuripotiwa katika mamlaka husika, hivyo kuonekana kama madhara ya UVIKO-19 kuwa madogo.
Bado wataalamu wanaendelea kutoa rai kwamba watu wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari zote za ugonja huu ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kunawa mikono mara kwa mara pamoja kuepuka kupeana mikono.