Juni 2021 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe aliulizwa na wanahabari kuhusu suala la kuazishwa kwa Mkoa mpya wa Chato na vigezo vinavyokubalika. Profesa Mdoe alinukuliwa akisema kuwa “Suala la kuanzisha Mkoa mpya lipo kwenye Mwongozo wa uanzishwaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wa 2014, hivyo TAMISEMI inafanya kazi kwa kufuata mwongozo huo na si vinginevyo.”
Mwongozo wa TAMISEMI unataja vigezo vya kuanzisha Mkoa mpya kuwa ni pamoja na eneo pendekezwa liwe na ukubwa wa kilometa za mraba zisizopungua 20,000, Wilaya nne, idadi ya watu wasiopungua asilimia 3 ya idadi ya Kitaifa (yaani watu watu milioni 1.7 kwa hesabu ya makadirio ya watu milioni 59.4).
Vigezo vingine ni idadi ya Tarafa zisizopungua 15, Kata zisizopungua 45, Vijiji visivyopungua 150, miundombinu ya uhakika kati ya makao makuu ya Mkoa na Wilaya zake, jiografia ambayo inafanya utoaji huduma kwa wananchi kuwa mgumu sababu ya milima, mito, misitu, mabonde au visiwa, uwezo wa Serikali kuanzisha pamoja na utayari wa wananchi kuchangia uanzisha
> Sababu za serikali kutositisha Mbio za Mwenge
Katiba Inaeleza Nini ?
Kwa mujibu wa Ibara 145 na 146 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, masharti na taratibu za kuanzishwa kwa mamlaka za Serikali za mitaa huzingatia mapendekezo au maombi ambayo lazima yapate ridhaa ya wananchi kupitia vikao vya kisheria.
Vikao vilivyoanishwa kwa mujibu wa utaratibu huo ni vya Vijiji, Kata (kamati ya maendeleo ya Kata-WDC), JJalmashauri kupitia baraza la Madiwani, Wilaya na Mikoa kupitia kamati za ushauri za wilaya (DCC) na ile ya Mkoa (RCC)
Ikiwa eneo fulani linakidhi matakwa na vigezo vyote vilivyoanishwa pamoja na wahusika kufuata taratibu zilizowekwa basi eneo hilo hutangazwa rasmi kuwa Mkoa mpya.