Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa watu 11 waliokutwa na hatia ya kumuua mwanaharakati wa ujangili, raia wa Afrika Kusini, Wayne Lotter.
Laila Mgonya, Jaji wa Mahakama Kuu ametoa hukumu hiyo jana Jumamosi Desemba 2,2022 baada ya kuridhika na ushahidi wa mashtaka uliothibitishwa pasina shaka na mashahidi 32.
Walio hukumiwa ni pamoja na Raia wawili wa Burundi Nduimana Ogiste na Habonimanda Nyandwi, Godfrey Salamba, Rahma Almas, Chambie Juma Ally, Allan Mafue, Ismail Mohammed, Leonard Makoi, Ayoub Kiholi, Abuu Mkingie, Muchael Kwavava.
Lotter alikuwa Mkurugenzi na Mwanzilishi-mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation lilokuwa likijihusisha na mapambano ya ujangili. Aliuawa Agosti 16, 2017 kwa kupigwa risasi na watu waliomvamia akiwa kwenye gari ndogo ya abiria, texi katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selaissie, Masaki wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.