Walimu 5,115 wa masomo ya sayansi wameajiriwa katika kipindi cha mwaka 2024/2025 na kuwa wamepangiwa katika maeneo yenye upungufu zaidi.
Naibu Waziri, Ofisi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba alibainisha hayo jana bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo (CCM) aliyetaka kufahamu juhudi gani zaidi Serikali inafanya kukabili tatizo la uhaba wa walimu hasa wa masomo ya Sayansi nchini.
Akijibu swali hilo, Katimba alisema Serikali inafanahamu tatizo la uhaba wa walimu hasa masomo ya sayansi nchini.
Alisema katika kukabiliana na uhaba huo Serikali imekuwa ikiajiri walimu wa kada mbalimbali, ikiwemo wa masomo ya sayansi kadiri ya upatikanaji wa fedha.
Aidha, Katimba alisema serikali itaendelea kuajiri walimu wa masomo ya sayansi kadiri ya upatikanaji wa fedha.