NZEGA: Wanachama 53 wa Chadema wahamia CCM

HomeKitaifa

NZEGA: Wanachama 53 wa Chadema wahamia CCM

Wanachama 53 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Nzega wametangaza kukihama chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakieleza kuwa CCM ndio chama cha siasa chenye nia thabiti ya kuwatumikia wananchi.

Kwa niaba ya wanachama wenzake, Shija Rajabu, alisema wametumikia Chadema kwa zaidi ya miaka 15, lakini chama hicho kimekuwa cha viongozi wa juu pekee ambao wanakiongoza kwa maslahi binafsi.

“CCM kwa sasa ndio chama cha siasa kilichobeba dhana zima ya utumishi bora uliotukuka haa kwa kutimiza ndoto za Watanzania masikini ambao siku zote wanahitaji huduma bora za afya,elimu,maji safi na miundombinu.

“Hata siku moja wananchi wa Nzega hatujawahi kufikilia kama kuna siku tutatumia maji ya Ziwa Viktoria lakini ilani ya CCM imejibu kwa vitendo kutoa maji Ziwa Viktoria mpaka kuwafikia watu wa Mkoa wa Tabora,” alisema Shija.

Aidha, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nzega, Amos Kanuda, alipongeza maamuzi waliyofanya wanachama hao wa Chadema kurudi CCM ambapo aliwahakikishia usalama na ushirikiano.

error: Content is protected !!