Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na mwekezaji wa klabu ya Simba , Mohamed Dewji ameshauri njia itakayoweza kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine kwani madhara yatokanayo na mgogoro huo ni makubwa na yanaathiri mataifa mengi.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mo Dewji aliandika kwamba Urusi na Ukraine wanapaswa kukaa na kumaliza tofauti zao kwani vita yao inasababisha ukosefu wa chakula bei ya bidhaa mbalimbali kupanda.
#Russia and #Ukraine should resolve their conflict through dialogue. The conflict has resulted in increased food shortages & prices. The two countries are the worlds top wheat producers. This would harm poor and developing continents including #Africa
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) May 3, 2022