Baada ya miaka 19 chini ya uongozi wa Roman Abramovich wa raia wa Urusi-Israeli, klabu ya mpira wa miguu ya Uingereza, Chelsea sasa kuhamia mkononi mwa mfanyabiashara bilionea, Todd Boehly.
ikiwa bado mali za Abramovich zimewekewa vikwazo, pesa zitokanazo na mauzo ya timu hiyo pia zitawekewa vikwazo hadi hapo itapobainika kuwa kweli zitatumika kusaidia wahanga wa vita huko Ukraine.
Umiliki wa klabu hiyo si wa Boehly pekee kwani kampuni ya Clearlake Capital huko California ndio inasemekana kuwa na hisa nyingi zaidi.
Wamiliki hao wapya wanapanga kuwekeza £1.75bn sawa na takribani trilioni tano za Kitanzania na kuifanya thamani ya jumla ya kununua klabu hiyo kufikia pauni 4.25bn
Serikali ya uingereza imesema “Hatua zilizochukuliwa leo zitahakikisha mustakabali wa mali hii muhimu ya kitamaduni na kulinda mashabiki na jumuiya pana ya soka. Tumekuwa katika majadiliano na washirika husika wa kimataifa kwa ajili ya leseni muhimu zinazohitajika na tunawashukuru kwa ushirikiano wao wote.”
Tangu 2003 chini ya uongozi wa Abramovich, Chelsea imefanikiwa kushinda makombe 21 ikiwemo makombe matano ya Ligi Kuu na mawili ya Ligi ya Mabigwa.