Ahukumiwa mwaka mmoja jela kwa wizi wa ndimu

HomeKitaifa

Ahukumiwa mwaka mmoja jela kwa wizi wa ndimu

Mahakama ya Wilaya Mwera imemhukumu Ramadhan Gere Shija (20) mkazi wa Bungi kutumikia Chuo cha Mafunzo kwa muda wa mwaka mmoja na kulipa faini ya Sh5,000 na fidia ya kima hicho hicho au kwenda jela miezi sita.

Hakima Rauhiya Hassan Bakar alitoa hukumu hiyo kwa mshtakiwa huyo baada ya kukubali kosa la wizi wa mazao.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Rauhiya alisema mahakama inamuona mshtakiwa huyo ni mkosa kisheria na kumpa adhabu hiyo, ili iwe fundisho kwake na watu wengine wenye tabia ya kujimilikisha vitu vya watu.

Kabla ya mahakama kutoa hukumu hiyo Mwendesha Mashitaka Wakili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Ali Juma aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa huyo alipatikana na kosa la wizi wa mazao kinyume na kifungu cha 251 (1)(2)(a) na 268 (1)(2)(3) cha sheria namba 6 ya mwaka 2018 sheria za Zanzibar.

error: Content is protected !!