Rais Samia atoa pole kwa Wajapani

HomeKimataifa

Rais Samia atoa pole kwa Wajapani

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Serikali ya Japan kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Shinzo Abe.

 Abe (67) alifariki dunia akiwa hospitali akipatiwa matibabu leo baada ya kupigwa risasi mara mbili ambapo moja imempata kifuani na nyingine mgongoni akiwa jukwaani akihutubia kwenye mji wa Nara nchini Japan katika kampeni za uchaguzi zinazoendelea nchini humo.

Katika salamu zake hizo, Rais Samia alizozituma leo Ijumaa Julai 8, 2022 kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameeleza kushtushwa na kifo cha Abe.

“Nimeshtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha Shinzo Abe aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan ambaye ni nguli jukwaani. Nitume salamu zangu za rambirambi kwa watu wa Japan’’ amendaka Rais Samia.

Abe, ambaye alikuwa Waziri Mkuu aliyekaa muda mrefu zaidi madarakani nchini Japan, alijiuzulu mwaka 2020 kwa kutoa sababu za kusumbuliwa kiafya.

Baada ya kujiuzulu alirithiwa na mshirika wake wa karibu Yoshihide Suga, ambaye baadaye nafasi yake ilichukuliwa na Fumio Kishida.

error: Content is protected !!