Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha na kuimarisha Taaluma kupitia michezo nchini kwa kutenga fedha kiasi cha Bil 2.1 kwaajili ya uendeshaji wa mashindano ya kimichezo kwa shule za Msingi (UMITASHUMNTA) na Sekondari (UMISSETA) nchini.
Akisoma taarifa yake tarehe 04 Agosti 2022 katika Ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMNTA na UMISSETA Mkoani Tabora Silinde amesema kuwa kwa mwaka 2022 Serikali imetenga Shilingi Bil.2.1 kwaajili ya uendeshaji wa mashindano ya kimichezo katika ngazi ya Msingi na Sekondari.
“Niendelee kuishukuru Serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha na kuimarisha michezo katika shule za Msingi, Sekondari kwa kutoa fedha zaidi ya Bil 2 kwaajili ya kuendesha mashindano haya,
“Fedha hizo zimetumika katika kuboresha miundombinu ya viwanja vya michezo pamoja na kuwawezesha wanafunzi na walimu nchini kushiriki mashindano yote yaliyopangwa bila kikwazo chochote na kwa ufanisi mkubwa” alisema Mhe. Silinde.
Aidha Mhe. Silinde amesema kuwa Serikali kupitia ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Elimu Sanyansi na Teknologia pamoja na Wizara ya Sanaa Tamaduni na Michezo imebainisha shule 56 nchini ambazo zitakuwa vituo vya kimichezo kwa wanafunzi wa Shule Msingi na Sekondari ili kuendeleza vipaji walivyonavyo pamoja na Taaluma zao.
“Kupitia Wizara za TAMISEMI, Elimu Sanyansi na Teknologia pamoja na Wizara ya Sanaa Tamaduni na Michezo tumeweza kubaini shule 56 ambazo zitakuwa vituo vya kimichezo kwa wanafunzi wetu ambao wana vipaji ambao watachaguliwa na Mikoa husika ili tuweze kuendeleza vipaji vyao” Mhe. Silinde
Vilevile Mhe. Silinde amesema kuwa Serikali imebainisha Mikoa ya Tanga, Mtwara na Tabora kama vituo vitatu vya kimichezoa mbapo katika Mikoa hiyo vitajengwa viwanja mseto(Multi sports) kwaajili ya kuratibu michezo nchini na tayari Katika Mkoa wa Tabora ujenzi wa viwanja hivyo unaendelea katika Shule za Sekondari Tabora Wavulana na Tabor