94.3% wakazi wa DAR wamehesabiwa

HomeKitaifa

94.3% wakazi wa DAR wamehesabiwa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema Mkoa huo umefanya vizuri kwenye zoezi la Sensa ya watu na Makazi ambapo mpaka asubuhi ya leo Agosti 30 zaidi ya asilimia 94.3 ya Wananchi walikuwa wamehesabiwa kulingana na taarifa zilizotumwa na Makarani wa zoezi hilo.

Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya mwenendo wa zoezi hilo, RC Makalla amesema Makarani ambao bado hawajakamilisha kutuma taarifa wakituma taarifa zote ni dhahiri kuwa Mkoa utakuwa umefikia asilimia 100.

Aidha RC Makalla amesema Mkoa huo unafanya Zoezi hilo kwa umakini mkubwa ili kupata takwimu sahihi na za uhakika Kutokana na Mkoa huo kuchukuwa asilimia 10-13 ya Wananchi wote wa Tanzania.

Ili kuhakikisha kila mmoja anahesabiwa, RC Makalla amewataka Wananchi ambao bado hawajahesabiwa kufika Ofisi za Serikali ya mtaa na kuacha mawasiliano au kupiga simu kupitia namba maalumu zilizotangazwa kwa kila Wilaya ili aweze kuhesabiwa.

Pamoja na hayo RC Makalla amempongeza Kamisaa wa Sensa Anna Makinda kwa kuongeza siku ambapo pia amewapongeza Wakuu wa Wilaya kwa kusimamia vizuri zoezi hilo.

error: Content is protected !!