Rais Samia azikumbusha nchi zilizoendelea kutimiza ahadi

HomeKitaifa

Rais Samia azikumbusha nchi zilizoendelea kutimiza ahadi

Rais Samia Suluhu amezitaka nchi zilizoendelea kutimiza ahadi ya kutoa fedha kwa nchi masikini kwa ajili ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema fedha hizo zitawasaidia kupata teknolojia za kisasa na kutekeleza miradi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi na changamoto zake.

Rais Samia amezitaka nchi hizo kuongeza juhudui za kutimiza malengo waliyoahidi ya kuzuia uzalishaji wa hewa ya ukaa, ili isiendelee kuleta madhara yatakayoshindwa kuilika na yanaoathiri nchi zinazoendelea kwa kiasa kikubwa.

Alisema hayo wakati akihutubia Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP27), jijini Sharmel El Sheikh, nchini Misri.

Alitaja mikakati ya kitaifa ya kukabiliana na athari ya tabianchi ni pamoja na kuzuia uzalishwaji wa hewa chafu kupitia uchumi kati ya asilimia 30 hadi 35 ifikapo mwaka 2030.

Kwa mujibu wa Rais Samia, Tanzania imejipanga kupanda miti milioni 200 kila baada ya miaka mitatu huku akiomba uwapo wa uwiano wa bei za kaboni duniani, ili kuzalisha rasilimali kutoka kwa njia hiyo.

 

error: Content is protected !!