80% ya kidato cha nne wafeli hesabu

HomeKitaifa

80% ya kidato cha nne wafeli hesabu

Licha ya kuongezeka kwa shinikizo la kuongeza ubora wa ufaulu katika masomo ya hesabu na sayansi nchini Tanzania miaka ya hivi karibuni, hali bado mbaya baada ya asilimia 80 ya watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne kufeli somo la hisabati.

Katika matokeo ya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2022, yaliyotangazwa jana Januari 29, 2023 na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) Athuman Amas ni asilimia 21.1 tu ya wanafunzi ndiyo wamefaulu somo hilo muhimu katika kumwandaa mwanafunzi kuwa na fikra tunduizi.

Hii ina maana kuwa ni watahiniwa wawili tu kati ya 10 waliofanya mtihani wa hisabati Novemba 2022 ndiyo wamefaulu.

Hesabu ni moja ya masomo muhimu katika ukuzaji wa sayansi na teknolojia katika taifa lolote ulimwenguni.

Kumekuwa na mfululizo wa matokeo mabaya katika somo la hisabati pamoja na masomo ya Sayansi katika matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi, upimaji kitaifa kidato cha pili na mtihani wa kuhitimu kidato cha nne.

“Katika somo la Basic Mathematics (Hisabati), watahiniwa 415, 844 wamepata daraja F ambao ni sawa na asilimia 79.9,” Amas amewaambia wanahabari jijini Dar es Salaam.

Hiyo inamaanisha kwamba wanafunzi nane kati ya 10 wamefeli somo hilo ambalo linatumika katika maisha ya kila siku.

error: Content is protected !!