Taasisi ya Elimu Tanzania imetoa mtaala wa elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la sita 2023.
Muundo wa mtaala huo umebadilika na sasa elimu hiyo itakuwa ni ya miaka sita badala ya saba kama ulivyokuwa Mtaala wa Elimu ya Msingi wa mwaka 2016.
Mtaala huo umezingatia nadharia za ukuaji na ujifunzaji na falsafa ya elimu ya kujitegemea inayosisitiza elimu inayomwezesha Mtanzania ajitegemee na amudu maisha yake ya kila siku.
Muundo wa mtaala unaonesha elimu ya msingi itatolewa kwa miaka sita katika hatua mbili ambazo ni darasa la kwanza na la pili ili kujenga umahiri katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Katika hatua ya pili inaonesha mtaala huo utaanzia darasa la tatu hadi la sita na italenga kuimarisha stadi za KKK na stadi nyingine za maisha.