Rais Samia: Tushirikiane kwenye uvumbuzi wenye manufaa

HomeKimataifa

Rais Samia: Tushirikiane kwenye uvumbuzi wenye manufaa

Rais Samia Suluhu Hassan amewasihi wakuu wa nchi na serikali mbalimbali kujikita zaidi kwenye uvumbuzi wenye manufaa ya kijamii na kiuchumi ili maendeleo yaweze kupatikana.

Amesema hayo alipikuwa akihutubia katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing nchini China.

“Uwepo wetu hapa leo unaonyesha mshikamano na dhamira ya kujenga mustakabali wa pamoja wa maendeleo na ustawi. Tushirikiane kwa uvumbuzi wenye manufaa kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya nchi zetu.” amesema Rais Samia Suluhu

Aidha, Rais Samia ameipongeza China kwa kuendelea kushirikiana na nchi za Afrika katika suala zima la kuondokana na umasikini na kueleza nia ya Tanzania na kuendeleza ushirikiano.

“Mchango wa China unaonekana wazi katika kuboresha miundombinu, kasi ya ukuaji wa viwanda, na maendeleo ya biashara ndogo na za kati katika nchi zetu. Kwa muktadha huu, Tanzania iko tayari kuwa mfano kwa ajili ya uvumbuzi wa kijamii na kiuchumi kati ya China na Afrika.” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!