BAKWATA yakemea upandishaji wa bei bidhaa kwenye mfungo

HomeKitaifa

BAKWATA yakemea upandishaji wa bei bidhaa kwenye mfungo

Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Wilaya ya Dodoma , Bashiru Omary amewataka wafanyabiashara kutotumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kama sehemu ya fursa ya kupandisha bidhaa zao kwa wateja wao.

Alitoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana, huku akiwataka wafanyabiashara kuelekea Ranadhani kujiepusha na upandishaji wa bei wa bidhaa zao.

Alisema mfungo wa Ramadhani si wote ambao wana kipato cha kuwawezesha katika kujikimu kimaisha ya kila siku, hivyo kitendo cha kupandisha bidhaa kinaweza kuwaumiza na kikanyima haki ya kufunga kama wengine.

“Kimsingi kitendo cha kupata faida kwa njia udhalimu isiyo halali kiungwana na siyo jambo jema mbele ya Mwenyezi Mungu, ukizingatia kuwa mwezi huo wa mfungo ni wa toba pamoja na kuwasaidia wale watakaoonekana hawajiwezi kiuchumi,” alisema.

Aidha, amewakumbusha waumini wenye kipato cha juu katika kuelekea kwenye mfungo huo wa Ramadhani kuwakumbuka wenye uhitaji na wasiojiweza kiuchumi.

error: Content is protected !!