Serikali imevuka lengo la ukuaji Pato la Taifa

HomeKitaifa

Serikali imevuka lengo la ukuaji Pato la Taifa

Wizara ya Fedha imesema imevuka lengo la ukuaji hali wa Pato la Taifa.

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema mwaka jana pato hilo lilikua kwa kiwango cha asilimia 5.5 ikilinganishwa na lengo la asilimia 5.4 na ukuaji asilimia 5.1 mwaka 2023.

Dk. Mwigulu alisema hayo bungeni Dodoma jana wakati akiwasilisha Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.

Alisema hadi Machi mwaka huu, akiba ya fedha za kigeni ilifika dola za Marekani milioni 5,693.2 na kwamba kiasi hicho kilitosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoa nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne.

Alisema pia, kati ya Julai mwaka jana hadi Aprili mwaka huu, mfumuko wa bei nchini ulifikia wastani wa asilimia 3.1 ikilinganishwa na asilimia 3.2 katika kipindi kama hicho mwaka 2023/2024.

Aliongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 shabaha za uchumi jumla zilizotarajiwa kufikiwa ni Pato la Taifa kufikia asilimia 5.4 mwaka 2024 kutoka ukuaji wa asilimia 5.1 mwaka 2023.

 

 

error: Content is protected !!