Serikali mbioni kuvipa vyombo vya habari ruzuku

HomeKitaifa

Serikali mbioni kuvipa vyombo vya habari ruzuku

Serikali imesema inatafakari kuona namna ya kufadhili vyombo vya habari kwa kuvipa ruzuku.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema vyombo vya habari ni sehemu muhimu katika jamii yoyote iliyostaarabika.

Profesa Kitila alisema hayo Dar es Saalam alipozungumza na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na waandishsi wa habari jana.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) inatambua na kuthamini mchango wa vyombo vya habari katika kukuza uwajibikaji na kuimarisha utawala bora nchini.

Profesa Kitila alisema dhamira ya serikali ya kuimarisha vyombo vya habari kwa kutoa ruzuku zitakazotokana na kodi za wanachi bila kuathiri uhuru wa habari.

Aidha, Profesa Kitila alisema lengo la serikali ni kuviwezesha vyombo vya habari kufanya kazi yake kwa ukweli, uwazi na kwa kuzingatia taaluma ya uandishi wa habari na si kuviimarisha viwe vinapendelea.

 

error: Content is protected !!