Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi zawadi ya Shilingi Bilioni 1 endapo timu ya Taifa, Taifa Stars, itatwaa ubingwa wa michuano ya CHAN 2024 inayoandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Palamagamba Aidan Mwaluko Kabudi, amesema ahadi hiyo inalenga kuongeza hamasa kwa wachezaji na mashabiki.
Waziri pia ametaja maandalizi muhimu ya mashindano, yakiwemo viwanja, malazi, usafiri na burudani kama tamasha la CHAN Singeli Festival. Aidha, kutakuwepo na zawadi ya “Goli la Mama” – Shilingi Milioni 10 kwa kila goli katika hatua ya makundi, na Milioni 20 kwa goli kwenye nusu fainali na fainali.
Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao chini ya kaulimbiu ya “LINAKUJA NYUMBANI”.