Wagombea ubunge CUF na CHAUMMA Lindi wahamia CCM

HomeKitaifa

Wagombea ubunge CUF na CHAUMMA Lindi wahamia CCM

Wagombea wawili wa Ubunge katika Jimbo la Mchinga mkoani Lindi kutoka vyama vya upinzani, wametangaza kuhama vyama vyao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakitaja sababu kuwa ni baada ya kuridhishwa na yaliyomo katika utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2025 – 2030.

Watia nia hao wametangaza uamuzi huo mbele ya mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye uwanja wa Ilulu mkoani Lindi ambaye amewapokea.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Lindi Mjini, mjumbe wa baraza kuu CUF taifa na mgombea wa ubunge Jimbo la Mchinga kupitia Chama cha wananchi CUF ndg,Rehema John Muhema leo amerudisha kadi na kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi.

Yusuph Issa Tamba, Mgombea Ubunge jimbo la Mchinga (CHAUMMA) ahamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wagombea hao ni Yusuph Issa Tamba kutoka Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) na Rehema John Muhema kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao walifuatana na wanachama wengine kutoka vyama vya upinzani akiwemo Salum Khalfan Baruani ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Lindi Mjini.

error: Content is protected !!