Venezuela kukabidhi kati ya mapipa milioni 30 hadi 50 ya mafuta kwa Marekani

HomeKimataifa

Venezuela kukabidhi kati ya mapipa milioni 30 hadi 50 ya mafuta kwa Marekani

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa Mamlaka za Mpito nchini Venezuela zitakabidhi kati ya mapipa milioni 30 hadi 50 ya mafuta ya ubora wa juu kwa Marekani. Trump amesema mafuta hayo, ambayo yalikuwa chini ya vikwazo, yatauzwa kwa bei ya soko la dunia.

Kupitia ujumbe alioutoa kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump ameandika mapato yatakayopatikana kutokana na mauzo ya mafuta hayo yatasimamiwa na ofisi ya Rais wa Marekani, yakilenga kunufaisha wananchi wa Venezuela na Marekani.

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha uwazi na matumizi sahihi ya fedha zitakazopatikana.

“Nimemwagiza Waziri wa Nishati wa Marekani, Chris Wright, kuanza utekelezaji wa mpango huo mara moja”. Ameandika Trump kwenye ujumbe huo.

Mafuta hayo yanatarajiwa kusafirishwa kwa meli maalum za kuhifadhi na kupelekwa moja kwa moja kwenye bandari za kupakulia mizigo nchini Marekani.

Ujumbe huo wa Trump unakuja wakati Venezuela ikiendelea kukabiliwa na changamoto za kiuchumi na kisiasa, huku Marekani ikisisitiza kushirikiana na mamlaka za mpito katika kusimamia rasilimali muhimu za taifa hilo.

error: Content is protected !!